Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba ameitaka jamii ya Kahama kuendelea kuunga mkono jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani uhitaji bado ni mkubwa. Ameyasema hayo mapema leo alipokuwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za Maendeleo katika Kata zake. Katika ziara hiyo ambayo ameongozana na timu yake ya Wataalamu (CMT) kikubwa kilichoonekana ni uhitaji wa Vyumba vya madarasa kwani kuna baadhi ya shule wanafunzi wanakaa zaidi ya 180 kwenye darasa moja kitu ambacho ni kiashiria cha kushuka kwa ufanisi katika ufundishaji.
"Kwa hali hii hata Malaika asingeweza kufundisha mwanafunzi aelewe, Mwalimu hawezi kufuatilia maendeleo ya Mwanafunzi mmoja mmoja kwa idadi hii ya wanafunzi, halafu Mwalimu ana vipindi vinne 'imagine' mzigo alio nao katika ufundishaji. Mwalimu wa hivi unawezaje kumpima kwenye OPRAS? Ni lazima tuweke mazingira mazuri ya ufundishaji ili kuwe na tija. Lakini niseme tu, nguvu ya Wananchi bado inahitajika, wajenge maboma hela ya kumalizia ipo. Mnapokuwa kwenye 'WDC' waleteni watu wajionee watoto zao wanavyokaa darasani, muyaongelee haya" Amesema Msumba.
Aidha amewataka wataalamu kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake kwani kuna mambo mengine ni lazima yashikiliwe na ngazi za juu.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa