Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack amehimiza ukamilishaji wa Hospitali ya Mji wa Kahama kwa kuzingatia viwango vya Ubora. Ametoa kauli hiyo mapema leo alipokuwa kwenye ziara ya Kikazi Wilayani hapa.
Bi.Telack amesema kuwa anatarajia kuona ujenzi unaenda kwa kasi na kwa kuzingatia viwango. Amesema kuwa ni kawaida na imezoeleka kuona ujenzi kuanza halafu ikifika katikati kulegalega kuna anza.
"Ni matarajio yangu kuona majengo haya yanaanza kazi Kabla ya 2020 yakiwa na ubora mkubwa. sitarajii kusikia Suma JKT imehama 'site' kwani imekua ni mazoea kwa wajenzi kupotea kabla kazi kuisha" Amesema Telack
Kwa Upande wake Msimamizi wa Ujenzi kutoka Jeshi la Kujenga Taifa 'Suma JKT" Bw. James amesema kuwa hadi sasa wako mbele ya kalenda hivyo ni matarajio yao kukamilisha ujenzi mapema iwezekanavyo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa