Wadau wa Maendeleo wa Wilaya ya Kahama leo wamehitimisha Warsha yao ya Siku mbili walizokutana ili kujadili Changamoto na fursa zilizopo Wilayani hapa.
Warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Kahama kuanzia jana tarehe 21/12/2020 hadi leo 22/12/2020 imehusisha Viongozi wa Wilaya ya Kahama na Wadau Wazawa wa Kahama waliopo maeneo mbalimbali duniani ambao wengine wameshiriki kwa njia ya Video.
Katika Warsha hiyo wadau hao wamejadili changamoto zilizopo Wilaya ya Kahama ambayo ina Halmashauri tatu (Ushetu, Msalala na Kahama Mji) na fursa zilizopo na namna ya kuzitumia ili kuleta maendeleo Chanya.
Mjadala ulikua unagusia sekta za Elimu, Afya, Miundombinu, Uchumi, Kilimo na Mifugo na huduma zingine za jamii zinazopatikana Wilayani humo.
Akifunga Warsha hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amewashukuru wadau hao kwa uamuzi wao wa kuungana na kuanzisha harakati hizo na amewaahidi kuwapa Ushirikiano wakati wowote watakapohitaji.
Wadau hao kwa mara ya Kwanza wameunganishwa na kundi la Whatsapp linaloitwa Kahama Kwetu na baadae wakaona haja ya kuunda umoja utakaotambulika rasmi kisheria "Society".
Baadhi ya Picha za tukio hilo hizi hapa:
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa